Firefox huhifadhi taarifa zako za kibinafsi kama vile alamisho, manenosiri na mapendeleo ya mtumiaji katika seti ya faili inayoitwa wasifu wako, ambayo huhifadhiwa katika eneo tofauti na faili za programu ya Firefox. Unaweza kuwa na wasifu nyingi za Firefox, kila moja ikiwa na seti tofauti ya taarifa za mtumiaji. Kidhibiti cha Wasifu (Profile Manager) kinakuruhusu kuunda, kuondoa, kubadilisha jina, na kubadilisha wasifu.
- Ikiwa una (au unapanga kuwa na) usakinishaji mwingi wa Firefox kwenye kompyuta moja, angalia Dedicated profiles per Firefox installation.
- Ikiwa unatatua tatizo la Firefox: Kipengele cha kuweka upya Firefox kinaweza kurekebisha matatizo mengi kwa kurejesha Firefox katika hali yake chaguomsingi huku kikihifadhi taarifa zako muhimu. Fikiria kutumia hivyo kabla ya kwenda kwa muda mrefu troubleshooting mchakato.
Table of Contents
Anzisha Kidhibiti cha Wasifu
Dhibiti wasifu wakati Firefox imefunguliwa
Andika about:profiles kwenye upau wa anwani na ubonyeze kitufe cha EnterReturn. Hii itafungua ukurasa wa Kuhusu Wasifu (About Profiles), ambapo unaweza kuona, kuunda na kudhibiti wasifu zako za Firefox.



Ukurasa wa Kuhusu Wasifu (About Profiles) unajumuisha chaguo zifuatazo:
- Bofya hii na ufuate maelekezo katika Oparesheni ya Kuunda Wasifu (Create Profile Wizard) (angalia sehemu ya Unda wasifu hapa chini kwa maelezo zaidi). Baada ya kumaliza kuunda wasifu mpya, itaorodheshwa kwenye Kidhibiti cha Wasifu. Wasifu mpya itakuwa chaguomsingi na itatumika wakati mwingine utakapoanzisha Firefox.
Ili kudhibiti wasifu, tafuta wasifu unaotaka kubadilisha na uchague kutoka kwa vitufe hivi chini ya wasifu huo:
- Bofya hii ili kubadilisha jina la wasifu kwenye Kidhibiti cha Wasifu. Kumbuka: Hii haibadilishi jina la folda iliyo na faili za wasifu huo.
- Bofya hii ili kufuta wasifu. (Wasifu unaotumika hauwezi kufutwa.) Usifute Faili (Don't Delete Files) ndilo chaguo linalopendelewa. Angalia sehemu ya Ondoa wasifu hapa chini kwa taarifa zaidi.
- Chaguo hili linakuruhusu kubadilisha wasifu. Bofya hii ili kufanya Firefox itumie wasifu huu kwa chaguomsingi inapoanza.
- Unapobofya hii, dirisha jingine la Firefox litafunguka kwa kutumia wasifu huo.
Anzisha Kidhibiti cha Wasifu wakati Firefox imefungwa
- Ikiwa Firefox imefunguliwa, funga Firefox: Bofya menyu ya Firefox
na uchague .Bofya menyu ya Firefox iliyo sehemu ya juu ya skrini na uchague .Bofya menyu ya Firefox
na uchague .
- Bonyeza kitufe cha Windows
+ R
+ R
+ R kwenye kibodi. Kisanduku cha mazungumzo cha Run kitafunguka.
- Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Run, andika:
firefox.exe -P
Unaweza kutumia-P,-pau-ProfileManager(yoyote kati ya hizo inapaswa kufanya kazi). - Bofya . Dirisha la Firefox la Chagua Wasifu wa Mtumiaji (Choose User Profile) linapaswa kufunguka.

Usakinishaji mwingi wa Firefox
Unaweza kuwa na programu nyingi za Firefox zilizosakinishwa katika maeneo tofauti. Ili kuanzisha Kidhibiti cha Wasifu kwa usakinishaji mahususi wa Firefox, badilisha firefox.exe katika maelekezo yaliyo hapo juu na njia kamili ya programu ya Firefox, weka mstari huo ndani ya alama za mnukuu, kisha uongeze nafasi ikifuatiwa na -P.
Mifano:
Firefox (32-bit) kwenye Windows ya 64-bit
"C:\Program Files (x86)\Mozilla Firefox\firefox.exe" -P
Firefox (32-bit) kwenye Windows ya 32-bit (au Firefox ya 64-bit kwenye Windows ya 64-bit)
"C:\Program Files\Mozilla Firefox\firefox.exe" -P
- Ikiwa Firefox imefunguliwa, funga Firefox: Bofya menyu ya Firefox
na uchague .Bofya menyu ya Firefox iliyo sehemu ya juu ya skrini na uchague .Bofya menyu ya Firefox
na uchague .
- Kwa kutumia Finder, nenda kwenye /Applications/Utilities.
- Fungua programu ya Terminal.
- Kwenye programu ya Terminal, ingiza yafuatayo:
/Applications/Firefox.app/Contents/MacOS/firefox -PKumbuka: Ikiwa programu yako ya Firefox iko katika eneo lingine tofauti naMuhimu: kuna nafasi baada ya njia, kabla ya/Applications/Firefox.app/, rekebisha ingizo hilo.-P(Unaweza kutumia-P,-pau-ProfileManagerbaada ya njia; yoyote kati ya hizo inapaswa kufanya kazi.) - Bonyeza Return. Dirisha la Kidhibiti cha Wasifu cha Firefox (Chagua Wasifu wa Mtumiaji) linapaswa kufunguka.
Ikiwa Firefox tayari imejumuishwa katika usambazaji wako wa Linux au ikiwa umesakinisha Firefox kwa kutumia kidhibiti cha vifurushi cha usambazaji wako wa Linux:
- Ikiwa Firefox imefunguliwa, funga Firefox: Bofya menyu ya Firefox
na uchague .Bofya menyu ya Firefox iliyo sehemu ya juu ya skrini na uchague .Bofya menyu ya Firefox
na uchague .
- Kwenye Terminal endesha:
firefox -P
Herufi P ni kubwa. Vinginevyo, unaweza kutumia -ProfileManager badala ya -P.
Dirisha la Kidhibiti cha Wasifu cha Firefox (Chagua Wasifu wa Mtumiaji) linapaswa kufunguka.
Ikiwa dirisha la Kidhibiti cha Wasifu bado halifunguki, huenda Firefox ilikuwa ikiendeshwa chinichini, hata kama haikuonekana. Funga matukio yote ya Firefox au uwashe upya kompyuta na kisha ujaribu tena.
Unda, ondoa au ubadilishe jina la wasifu
Unaweza kuunda, kuondoa au kubadilisha jina la wasifu aidha kutoka kwenye dirisha la Chagua Wasifu wa Mtumiaji wakati Firefox imefungwa au kutoka kwenye ukurasa wa Kuhusu Wasifu wakati Firefox imefunguliwa, kama ifuatavyo:
Unda wasifu
- Bofya kitufe cha kwenye dirisha la Chagua Wasifu wa Mtumiaji (Choose User Profile), au ubofye kitufe cha kwenye ukurasa wa Kuhusu Wasifu (About Profiles), ili kuanzisha Oparesheni ya Kuunda Wasifu.
- Bofya na uingize jina la wasifu. Tumia jina la wasifu linaloelezea vyema, kama vile jina lako la kibinafsi. Jina hili halitawekwa wazi kwenye Intaneti.
- Puuza chaguo la isipokuwa kama ungependa kuchagua folda mahususi ya kutumia kwa wasifu wako mpya.Onyo: Ukichagua kuunda wasifu katika eneo jipya kwenye kompyuta yako, chagua folda mpya au tupu. Ukichagua folda ambayo si tupu na baadaye ukaondoa wasifu na kuchagua chaguo la Futa Faili (Delete Files), kila kitu kilicho ndani ya folda hiyo kitafutwa.
- Ili kuunda wasifu mpya, bofya .
Utarudishwa kwenye dirisha la Chagua Wasifu wa Mtumiaji au ukurasa wa Kuhusu Wasifu na wasifu mpya utaorodheshwa. Unapoanzisha Firefox kwa mara ya kwanza ukitumia wasifu mpya, utaombwa kuingia katika Mozilla account yako ili uweze kusawazisha data yako na wasifu mpya (angalia hapa chini).
Ondoa wasifu
Unaweza kuondoa wasifu uliopo kama ifuatavyo:
- Chagua wasifu wa kuondoa na ubofye kwenye dirisha la Chagua Wasifu wa Mtumiaji, au ubofye kitufe cha kwenye ukurasa wa Kuhusu Wasifu chini ya jina la wasifu unaotaka kufuta.
- Thibitisha kuwa ungependa kufuta wasifu huo:
- huondoa wasifu kutoka kwenye Kidhibiti cha Wasifu lakini hubakiza faili za data ya wasifu kwenye kompyuta yako katika folda ya hifadhi, ili taarifa zako zisipotee. Usifute Faili (Don't Delete Files) ndilo chaguo linalopendelewa kwa sababu linahifadhi folda ya wasifu wa zamani na kukuruhusu kurejesha faili hizo kwenye wasifu mpya.
- huondoa wasifu na faili zake (ikijumuisha alamisho za wasifu, mipangilio, manenosiri, n.k.). Ukitumia chaguo la Futa Faili (Delete Files), folda ya wasifu na faili zitafutwa. Kitendo hiki hakiwezi kutenduliwa.
- hukatiza ufutaji wa wasifu.
Badilisha jina la wasifu
Unaweza kubadilisha jina la wasifu kama ifuatavyo:
- Chagua wasifu wa kubadilisha jina kwenye dirisha la Chagua Wasifu wa Mtumiaji na ubofye au ubofye kitufe cha kwenye ukurasa wa Kuhusu Wasifu chini ya wasifu unaotaka kubadilisha jina.
- Ingiza jina jipya la wasifu. Andika jina jipya la wasifu, na ubofye .
- Kumbuka: Folda iliyo na faili za wasifu huo haibadilishwi jina.
Chaguo
Chaguo hizi zinapatikana tu unapo anzisha Kidhibiti cha Wasifu wakati Firefox imefungwa.
Fanya kazi Nje ya Mtandao
Kuchagua chaguo hili kunapakia wasifu uliochaguliwa na kuanzisha Firefox bila kuunganisha kwenye Intaneti. Unaweza kuona kurasa za wavuti zilizotazamwa awali na kufanya majaribio na wasifu wako.
Tumia wasifu uliochaguliwa bila kuuliza inapoanza
Unapokuwa na wasifu nyingi, chaguo hili linaiambia Firefox nini cha kufanya inapoanza:
- Ukiweka tiki kwenye chaguo hili, Firefox itapakia kiotomatiki wasifu uliochaguliwa inapoanza. Ili kufikia wasifu nyingine, lazima uanzishe Kidhibiti cha Wasifu kwanza.
- Ukiondoa tiki kwenye chaguo hili, Firefox itakuonyesha Kidhibiti cha Wasifu kila wakati unapoanzisha Firefox, ili uweze kuchagua wasifu wa kutumia.
Tumia Sync na wasifu mpya
Unaweza kusawazisha wasifu wako mpya na wasifu na vifaa vingine vya Firefox. Ili kujifunza zaidi, angalia How do I set up Sync on my computer? na Nitachaguaje maelezo ya kusawazisha kwenye Firefox?
Hamisha wasifu
Ili kunakili data na mipangilio yako yote ya Firefox kwenda kwenye usakinishaji mwingine wa Firefox (kwa mfano, unapopata kompyuta mpya), unaweza kufanya chelezo ya wasifu wako wa Firefox, kisha uirejeshe katika eneo lako jipya. Kwa maelekezo, angalia Manually back up and restore Firefox profile data.
Rejesha taarifa kutoka kwenye wasifu wa zamani
Ikiwa una taarifa muhimu kutoka kwenye wasifu wa zamani wa Firefox, kama vile alamisho, manenosiri au mapendeleo ya mtumiaji, unaweza kuhamisha taarifa hizo kwenda kwenye wasifu mpya wa Firefox kwa kunakili faili zinazohusiana. Kwa maelekezo, angalia Restore bookmarks, passwords and data from an old Firefox profile. Unaweza pia kubadilisha kwenda kwenye wasifu wa awali ili kurejesha data ya wasifu wa zamani. Angalia Recover user data missing after Firefox update or reinstall kwa maelezo zaidi.