Jinsi ya kushusha na kufunga Firefox juu ya Mac

Makala hii inaeleza jinsi ya kushusha na kufunga Firefox juu ya Mac..

Kumbuka: Makala hii inatumika tu kwa Mac. Kwa maelekezo ya kufunga Firefox juu ya Windows, angalia Jinsi ya kushusha na kufunga Firefox katika Windows.Kwa maelekezo ya kufunga Firefox juu ya Linux, angalia Install Firefox on Linux.
Hakikisha Mac yako inapita Mahitaji ya Mfumo. Ikiwa unatumia toleo la kale la Mac OS, tazama makala haya kwa maelezo zaidi *Firefox support has ended for Mac OS X 10.6, 10.7 and 10.8.

Kufunga Firefox juu ya Mac

 1. Tembelea ukurasa wa kushusha Firefox katika kivinjari yoyote (kwa mfano, Apple Safari). Hiyo moja kwa moja itachunguza jukwaa na lugha kwenye kompyuta yako na kupendekeza toleo bora ya Firefox kwa ajili yako.
 2. Bonyeza kifungo cha kijani kushusha Firefox.
  download page mac
 3. Mara shusha imekamilisha, faili ya (Firefox.dmg) inapaswa kufungua peke yake na hapo kufungua dirisha la Finder zenye programu za Firefox. Kokota ikoni ya Firefox juu ya folda ya Programu ili kuunakili huko.
  fxmacinstall
  Kumbuka:Kama hauoni dirisha hii, bofya failiya Firefox.dmg iliyopakuliwa kuifungua.
  Mac Install 2
 4. Baada ya kukokota Firefox kwa folda ya Programu, shikilia chini kitufe cha control huku ukibofya katika dirisha na kuchagua Eject "Firefox" kutoka orodha.
  Mac Install 4
 5. Unaweza kuongeza Firefox kizimbani mwako kwa urahisi. Fungua folda ya Programu yako na ukukote Firefox hadi kizimbani.
  Add to Dock
  Firefox ipo tayari kwa matumizi. Bonyeza tu juu ya picha yake kizimbani kuanzisha.

Kuanzia Firefox kwa mara ya kwanza

Wakati unpoanzisha Firefox kwa mara ya kwanza, utapewa onyo kwamba Firefox ilipakuliwa kutoka kwa mtandao. Kwa sababu wewe ulishusha Firefox kutoka tovuti rasmi, unaweza bonyeza Open.

Firefox Downloaded Security Check Mac

Pia, Firefox haitakuwa kivinjari cha msingi kwako na utaambiwa kuhusu jambo hilo. Hiyo ina maana kwamba wakati wa kufungua kiungo katika programu ya barua pepe yako, njia ya mkato ya mtandao, au hati ya HTML, 'haitafunguliwa' katika Firefox. Kama unataka Firefox kufanya mambo hayo, bonyeza kifungo Use Firefox as my default browser ili kuweka kama default browser yako. Kama sivyo au unajaribu tu Firefox, bonyeza kifungo Sio Sasa.

Firefox as Default Browser Dialogue Mac

Makala hii ilikuwa na umuhimu?

Tafadhali subiri...

These fine people helped write this article:

Illustration of hands

Volunteer

Grow and share your expertise with others. Answer questions and improve our knowledge base.

Learn More