Badilisha lugha msingi katika Firefox kwa iOS

Firefox itabadili kwa lugha yoyote ya iPad, iPhone iPod au vifaa vya kugusa utakayoweka, hivyo unaweza kubadili lugha bila kushusha Firefox tena. Hapa ni jinsi ya kufanya hivyo:

  1. Nenda kwa program ya Settings kwenye iPad au iPhone.
  2. Bomba General.
  3. Bomba Language & Region.
  4. Bomba iPad/iPod/iPhone Language kuona chaguo zako.
  5. Bomba lugha unataka kutumia, ikifuatiwa naDone.

Ipatie kifaa chako sekunde chache ili kubadili kabla ya kufungua Firefox.

Tazama Je, Firefox inapatikana kwa iPhone au iPad? kwa orodha ya lugha zilizopo.
// These fine people helped write this article:Michael Buluma. You can help too - find out how.

Makala hii ilikuwa na umuhimu? Tafadhali subiri...

Jitolee kwa ajili ya Mozilla Support