Kusaini Add-on katika Firefox

Add-ons zinazobadilisha mazingira ya browser yako bila idhini yako au kuiba taarifa yako wameongezeka zaidi. Baadhi ya add-ons huongeza toolbars zisizohitajika au vifungo, mabadiliko ya mazingira yako ya utafutaji au kuingiza matangazo au programu hasidi kwenye kifaa chako. Makala hii inaeleza jinsi kusaini add-ons inakulinda dhidi ya vitisho kama hivyo.

Kusaini add-ons ni nini?

Mozilla inathibitisha na "kusaini" add-ons zinazofuata seti ya miongozo ili kuhakikisha kuwa taarifa za watumiaji haiwezikuibiwa au kuvurugwa. Add-ons zote zilizopangishwa kwenye addons.mozilla.org hupitia mchakato na mapitio ili kuthibitishwa na kutiwa saini. Add-ons zilizopangishwa kwenye maeneo mengine zitahitaji kufuata miongozo hiyo ili kusainiwa na Mozilla.

Kuongeza-on kusaini 'hulenga programu hasidi tu na browser utekaji nyara' . Haina udhibiti au kuchuja maudhui ambayo wewe unachagua kuona.

Watengenezaji: Jifunze zaidi kuhusu miongozo ya add-on kusainiwa kwa Mozilla Developer Network.

Nini naweza kufanya ikiwa Firefox inalemaza add-on iliyowekwa, isiyosainiwa?

Kama yoyote ya add-ons zilizowekwa kwako zinapata kulmelemazwa kwa sababu hazijawahi kuthibitishwa, wasiliana na mtengenezaji wa add-on au muuzaji ili kuona kama wanaweza kutoa toleo jipya na kusaini toleo hilo la add-on. Unaweza pia kuwauliza wapate kutia saini add-on zao..

Kubatilisha kusaini add-on (watumiaji wa juu): Unaweza kupuuza mpangilio huu kwa kubadilisha xpinstall.signatures.required mpangilio kuwa false katika kihariri cha usanidi wa Firefox (ukurasa wa about:config). Msaada haupatikani kwa mabadiliko yoyote yaliyotolewa na uhariri wa Usanidi kwa hivyo tafadhali kufanya hivi katika hatari yako mwenyewe.

Ni kwa jinsi gani kusaini add-on inanilinda mimi?

Firefox inakulinda wewe dhidi ya programu hasidi na watekaji wa browser kwa kuruhusu tu add-ons zilizothibitishwa na kutiwa saini kidigitali kuwekwa katika kivinjari chako.

Firefox inakulinda wewe dhidi ya programu hasidi na browser watekaji na onyo kuhusu add-ons ambazo hazijathibitishwa na kutiwa saini kidigitali na Mozilla.

Kutumia kipengele hii mpya, tafadhali sasisha kwa toleo la karibuni la Firefox

Matoleo mapya ya Firefox yatakulinda dhidi ya programu hasidi na watekaji wa browser na onyo kuhusu na (kuanzia Firefox 43) kuzuia add-ons ambazo hazijathibitishwa na kutiwa saini kidigitali na Mozilla.

Wakati Firefox ya sasa ina mfumo wa orodha ya kuzuia , inazidikuwa vigumu kufuatilia na kuzuia idadi inayoongezeka ya add-ons hasidi. Mchakato mpya wa Add-ons kusainiwa inahitaji watengenezaji kufuata kanuni za Mozilla Developer na kuhakikisha kwamba add-ons zaho ni salama. Firefox hukuonya wakati add-on haikuweza kukamilisha mchakato wa kutia saini. Kwa sasa bado unaweza kufunga add-ons zisizokuwa na ushahidi kwa hasara yako mwenyewe, lakini kuanzia na Firefox 43, add-ons hizi zitapata kulemazwa pia.

Sakinisha add-ons tu kutoka kwa watengenezaji unao waamini. Add-ons ambazo hazijathibitishwa zinaweza kujumuisha programu hasidi au watekaji ambao wanaweza kubadilisha mazingira yako na kuiba taarifa yako.

Ni aina gani ya add-ons zinahitajika kuwa na saini?

Extensions (add-ons ambazo zinaongeza makala kwa Firefox) zitahitaji kutiwa saini. Mandhari, vikundi vya lugha na Plugins hazihitaji kuwa na saini.

Ni wapi naweza kukutana na add-ons isiyosainiwa?

Add-ons zilizowekwa kupitia tovuti rasmi ya Firefox Add-ons hupitia mchakato kali wa mapitio kabla ya kuchapishwa. Add-ons hizi zimethibitishwa na kutiwa saini.

Unaposakinisha add-on kwa njia ya tovuti nyingine, Firefox huangalia ili kuhakikisha kuwa add-on imetiwa saini kitarakimu kabla unaweza kufunga hiyo.

// These fine people helped write this article:Michael Buluma. You can help too - find out how.

Makala hii ilikuwa na umuhimu? Tafadhali subiri...

Jitolee kwa ajili ya Mozilla Support