Jinsi ya kushusha na kufunga Firefox juu ya Mac

Revision Information
  • Revision id: 103901
  • Ilibuniwa:
  • Muumba: Michael Buluma
  • Comment: en to sw
  • Reviewed: Ndio
  • Reviewed:
  • Reviewed by: buluma_michael
  • Is approved? Ndio
  • Is current revision? La
  • Ready for localization: La
Revision Source
Revision Content

Makala hii inaeleza jinsi ya kushusha na kufunga Firefox juu ya Mac..

Kumbuka: Makala hii inatumika tu kwa Mac. Kwa maelekezo ya kufunga Firefox juu ya Windows, angalia Jinsi ya kushusha na kufunga Firefox katika Windows.Kwa maelekezo ya kufunga Firefox juu ya Linux, angalia Install Firefox on Linux.
Firefox inahitaji Intel processor na Mac OS X 10.5 au ya juu hadi Firefox 16, Mac OS X 10.6 au ya juu kutoka Firefox 17. Tazama Mahitaji ya Mfumo. Ikiwa unatumia toleo la kale la Mac OS , tazama Firefox no longer works with Mac OS X 10.4 or PowerPC processors au Firefox no longer works with Mac OS X 10.5 kwa msaada.

Kufunga Firefox juu ya Mac

  1. Tembelea http://mozilla.org/firefox katika kivinjari yoyote (kwa mfano, Apple Safari). Hiyo moja kwa moja itachunguza jukwaa na lugha kwenye kompyuta yako na kupendekeza toleo bora ya Firefox kwa ajili yako.
  2. Bonyeza kifungo cha kijani kushusha Firefox.
    Mac Install 1
  3. Mara shusha imekamilisha, faili ya (Firefox.dmg) inapaswa kufungua peke yake na hapo kufungua dirisha la Finder zenye programu za Firefox. Kokota ikoni ya Firefox juu ya folda ya Programu ili kuunakili huko.
    Mac Install 2a
    Kumbuka:Kama hauoni dirisha hii, bofya failiya Firefox.dmg iliyopakuliwa kuifungua.
    Mac Install 2
  4. Baada ya kukokota Firefox kwa folda ya Programu, shikilia chini kitufe cha control huku ukibofya katika dirisha na kuchagua Eject "Firefox" kutoka orodha.
    Mac Install 4
  5. Unaweza kuongeza Firefox kizimbani mwako kwa urahisi. Fungua folda ya Programu yako na ukukote Firefox hadi kizimbani.
    Add to Dock
    Firefox ipo tayari kwa matumizi. Bonyeza tu juu ya picha yake kizimbani kuanzisha.

Kuanzia Firefox kwa mara ya kwanza

Wakati unpoanzisha Firefox kwa mara ya kwanza, utapewa onyo kwamba Firefox ilipakuliwa kutoka kwa mtandao. Kwa sababu wewe ulishusha Firefox kutoka tovuti rasmi, unaweza bonyeza Open.

installingonmac-5-jpg60.jpg

Kumbuka: Ukiona ujumbe "Firefox.app" can't be opened because the identity of the developer cannot be confirmed tazama Firefox can't be opened after you install it on a Mac - How to fix kwa ufumbuzi.

Pia, Firefox haitakuwa kivinjari cha msingi kwako na utaambiwa kuhusu jambo hilo. Hiyo ina maana kwamba wakati wa kufungua kiungo katika programu ya barua pepe yako, njia ya mkato ya mtandao, au hati ya HTML, 'haitafunguliwa' katika Firefox. Kama unataka Firefox kufanya mambo hayo, bonyeza kifungo Yes ili kuweka kama default browser yako. Kama sivyo au unajaribu tu Firefox, bonyeza kifungo La.

installingonmac-6-jpg60.jpg